LIVERPOOL: Shirikisho la soka nchini England limelaani vikali vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyojitokeza katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi hiyo Ijumaa usiku mchezo uliohusisha mabingwa watetezi Liverpool dhidi ya Bournemouth mchezo uliomalizika kwa Liverpool kushinda mabao 4-2
Mchezo huo ulisimama kwa muda baada ya mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Ghana Antoine Semenyo kuripoti kwa muamuzi Anthony Taylor ambaye alisimamisha mchezo huo dakika ya 29 wakati Liverpool ikipiga kona kuelekea Bournemouth
Taylor aliwaita makocha wa timu zote kwenye touchline na kuzungumza nao kuwaarifu juu ya jambo hilo kisha kuzungumza na manahodha Virgil Van Dijk na Adam Smith kuwapa maelekezo.
Asubuhi ya leo Jumamosi Premier league ilitoa taarifa ya kulaani tukio hilo na kusisitiza kuwa vitendo hivyo havina nafasi katika ligi hiyo ambayo ni ya kila mchezaji na ya kila shabiki
“Tuna wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa vitendo vya ubaguzi kutoka kwenye eneo la mashabiki”
“Matukio ya aina hii hayana nafasi katika mchezo wetu, na tutashirikiana kwa karibu na wasimamizi wa mechi, klabu na mamlaka husika ili kubaini ukweli na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.” – ilisema taarifa ya Premier League.
Polisi wa Merseyside wamesema mwanamume mwenye umri wa miaka 47 alifukuzwa Anfield baada ya ripoti za ubaguzi huo, na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea. Liverpool walisema wataunga mkono kikamilifu uchunguzi wa polisi
The post Premier League yaapa kumaliza ubaguzi wa mashabiki first appeared on SpotiLEO.