Burudani za CHAN 2024 zinaendelea hii leo kwa michezo miwili muhimu kupigwa kwenye Kundi A, mechi zote mbili zitapigwa mapema majira ya saa 9 Alasiri katika viwanja viwili tofauti.
Kwenye dimba la Nyayo utapigwa mchezo kati ya DR Congo dhidi ya Morocco, timu zote zikiwa na alama 6 na kuwania nafasi ya kuungana na Kenya kucheza Robo Fainali.
Wakati kule Moi Kasarani vinara wa Kundi A, watakuwa na kibarua cha kuisaka nafasi ya kuongoza Kundi hilo wakikipiga dhidi ya Zambia ambao tayari wameaga mashindano hayo.
Kenya tayari wamefuzu hivyo kibarua pekee ni kusaka alama zitakazofanya waongoze Kundi A, wakati vita kubwa ipo kati ya DR Congo na Morocco wanaotafuta alama zitakazowapa uhakika wa kutinga hatua inayofuata.
Ikumbukwe kuwa mpinzani wa Stars kwenye hatua ya Robo Fainali anapatikana katika Kundi hili.