CHADEMA: YANGA IKUMBANE NA RUNGU LA FIFA
CHADEMA wameitumia FIFA barua rasmi ya malalamiko yao dhidi ya Klabu ya Yanga wakihusishwa kuwa na Ushirika wa karibu na CCM katika barua hiyo iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Chama hicho ni kuwa wameweka matakwa yafuatayo:
1- Uchunguzi ufanywe na FIFA kuhusu ushirika wa Yanga katika masuala ya kisiasa.
2- Yanga ikumbane na rungu mara moja kama klabu lakini Viongozi wake pia wapokee adhabu kali kulingana na taratibu za FIFA.
3- Kusisitiza na kuzuia soka la Tanzania kushirikiana na masuala ya kisiasa.
CHADEMA wapo tayari wakati wowote kutoa Ushahidi pale ambapo FIFA watahitaji.