Ameandika ahmed ally
Tunakwenda kwenye hatua ya Robo Fainali ya CHAN dhidi Morocco August 22
Lazima tukiri kuwa hatua ya Makundi haikua bora kwetu kwenye upande wa majukwaa
Pamoja na timu yetu kuwa ndio timu iliyofanya vizuri kuliko zote lakini haijapata thamani sawa ya ubora huo na muitikio wa mashabiki
Sio muda wa kushikana uchawi bali ni muda wa kila mtu kutimiza majukumu yake
Kwenye kutimiza majukumu, Niwaombe ndugu zangu Waandishi wa habari nyie ni kiungo muhimu sana kwenye kufanikisha jambo lolote lile
Kwenye vipindi vyenu vya michezo ipeni nafasi Stars, tengenezeni morali kwa mashabiki na muwaite mashabiki waje Uwanjani
Watu mashuhuri wa kada zote tuibebe Agenda hii ya Taifa, tutumie nafasi zetu kuhamasisha mashabiki wetu twende Uwanjani
Mechi ya Robo Fainali tuvunje rekodi yetu ya kuingia Uwanjani na hilo linawezekana sana
Viongozi wa Matawi ya Simba, Azam, KMC na Yanga tumieni Matawi yenu kuhamasisha Wanachama wenu kuja kwa wingi Uwanjani
Vile mnfanya panapokua na mechi za vilabu vyetu tufanye hivyo hivyo kwa Taifa letu.
Ijumaa August 22 twendeni tukaujaze Benjamini Mkapa