Klabu ya ENPPI ya ligi kuu Nchini Misri imetangaza kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa siku ya jana jijini Cairo, Misri.
Klabu ya Simba ilishiriki kwenye mchezo huo kwa mualiko maalum wa klabu hiyo katika sherehe za miaka 40 ya kuanzishwa kwa klabu ya hiyo ya ENPPI.
Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Jenerali Richard Makenzo, akishirikiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ENPPI, Bwana Ayman Al-Shari.
Licha ya kuwa klabu ya Simba haijathibitisha kucheza mchezo huo lakini timu ya Enppi imethibitisha hilo kupitia ukurasa wao wa Instagram walipoambatanisha na picha za matukio ya mchezo huo.