TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Agosti 22 2025 ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Morocco ikiwa ni CHAN 2024.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa mbili usiku huku benchi la ufundi la Stars likibainisha kuwa lipo tayari kuhakikisha matokeo yanapatikana ndani ya dakika 90.
Hemed Suleman, Kocha Mkuu wa Stars amesema wanatambua kwamba mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na ugumu wa hatua waliyopo lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.
“Nimefarijika kuona tunatengeneza nafasi suala la kutuma nafasi bado tunaendelea kuhakikisha tunapamana nalo, kabla ya mashindano nilisema kuna changamoto katika umaliziaji lakini nashukuru tunaendelea vizuri tumefunga mabao matano katika hatua ya makundi.
“Tunarudi katika robo fainali ni mechi ya maamuzi tunatkiwa kufunga magoli kwahiyo wachezaji wanaendelea kufanya mazozi ya kuona kila nafasi tunayopata tunaitumia. Wapinzani tunawaheshimu hivyo tutahakikisha tunapata matokeo kenye mchezo wetu muhimu.”