Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Crystal Palace raia wa Uingereza Eberechi Eze ni rasmi amesaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Arsenal kilichosalia tu ni utambulisho.
Siku ya jana nyota huyo aliripotiwa kufanya vipimo vya afya na leo mapema taarifa kutoka Uingereza zinaripoti kuwa nyota huyo amesaini kuitumikia klabu hiyo ya ndoto zake na muda wowote atatambulishwa.