Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Bukayo Saka huwenda akakosekana uwanjani kwa kipindi cha wiki tatu hadi wiki nne baada ya kupata jeraha la misuli ya paja ‘hamstring’ katika mchezo dhidi ya Leeds United.
Taarifa za awali ambazo bado hazijathibitishwa na klabu yake Saka zinaripoti kuwa nyota huyo atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne akiuguza jeraha lake baada ya kuumia katika mchezo huo.