Timu ya Taifa ya Madagascar imetinga fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN2024 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan kwenye nusu fainali licha ya kucheza kwa zaidi ya dakika 49 ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja.
Kiungo Fenohasina Razafimaro wa Madagascar alioneshwa kadi nyekundu mnamo dakika ya 79 lakini timu yake imekuwa timu ya kwanza kutinga fainali ya CHAN2024 na itachuana na mmoja kati ya Morocco au Senegal.
FT: Madagascar π²π¬ 1-0 πΈπ© Sudan
π₯ 79β Razafimaro
β½ 116β Rakotondraibe
βΒ