ALIYEKUWA beki wa kushoto wa Yanga SC, Nickson Kibabage tayari amejiunga na Singida Black Stars kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya mara baada ya kuachana na timu hiyo, katika msimu ujao.
Beki huyo alikuwa katika kikosi cha Yanga SC msimu wa 2024/25. Alitwaa taji la ligi chini ya Kocha Mkuu Miloud Hamdi ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi hicho.
Timu hiyo inanolewa na Romain Folz ambaye ni raia wa Ufaransa kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya msimu mpya 2025/26.
Inaelezwa kuwa taratibu zote za uhamisho wa beki huyo aliyempisha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyejiunga na Yanga SC kwa mkataba wa miaka miwili ambaye kwa sasa atakuwa kwenye changamoto mpya.
Kibabage hakuwa chaguo la kwanza msimu uliopita kwenye mechi 30 za ligi alipata nafasi ya kucheza jumla ya mechi 12 pekee msimu wa 2024/25.
Katika mechi hizo 12 alikomba jumla ya dakika 889, hivyo huenda akawa kwenye changamoto mpya msimu ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ikumbukwe kwamba anarejea kwenye timu ambayo aliwahi kucheza kabla ya kujiunga na Yanga SC.