Dili la beki wa Crystal Palace Marc Guehi kwenda Liverpool limekwama baada ya Crystal Palace kukosa mbadala wake dakika za mwisho kabla dirisha la usajili kufungwa hivyo nyota huyo raia wa England anarejea London.
Guehi 25, alikuwa tayari amekamilisha vipimo vya afya na kufikia makubaliano ya mkataba wa miaka mitano wa kujiunga na Liverpool lakini dili limekufa baada ya Palace kumkosa beki wa Brighton Igor Julio aliyeamua kujiunga na West Ham United.
Habari za kukwama kwa dili hilo ni njema kwa kocha wa Palace Oliver Glasner ambaye awali aliitaka klabu hiyo isikubali kumuuza beki huyo kwani ni sehemu muhimu kwa ajili ya mafanikio ya klabu hiyo.