Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amethibitisha kuwa siku ya kesho watawakosa wachezaji wawili katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Yanga wachezaji hao ni Mohamed Bajaber na Alassane Kante.
“Bajaber ana majeraha, Allasane Kante naye pia aliumia kwenye pre season hivyo hao wawili wataukosa mchezo wa Yanga lakini Semfuko naye alikuwa ana majeraha japo amerejea mazoezini sasa hivyo yeye anaweza kuwepo kwenye mchezo huo ” – Fadlu Davids, Kocha Simba SC.