DAR ES SALAAM:MSANII wa filamu za Bongo, Blandina Chagula maarufu kama Johari, amewajibu wanaomcheka na kudai kuwa hana uwezo wa kuzaa, kwa kuwaonesha mtoto wake mwenye umri wa miaka 8.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Johari ameweka picha ya mtoto wake na kuandika:
“Pole yenu mnaodhani mimi ni mgumba sina mtoto, sina kizazi. Kwa taarifa yenu nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka minane (8).”
Muigizaji huyo ameeleza kuwa ameamua kufunguka baada ya maneno ya mitandaoni kuenea yakimchafua kwamba hawezi kupata mtoto.
Amesisitiza kuwa mtoto ni bahati na baraka kutoka kwa Mungu, hivyo si vyema kuwabeza au kuwakejeli wasio nao, bali kuwaombea ili kwa wakati wa Mungu nao wapate baraka hiyo.
The post Johari awavaa wanaomsema hana mtoto first appeared on SpotiLEO.