MUNICH: MSHAMBULIAJI wa Chelsea Cole Palmer amesema klabu hiyo haiitazami kampeni yao Ligi ya Mabingwa ulaya (UCL) msimu huu kama safari ya kujifunza kwa sababu wanataka kutoa ushindani haraka ikiwezekana kutwaa kombe hilo.
Vijana wa Enzo Maresca walikubali kuwa timu ya pili walipopoteza kwa mabao 3-1 mbele ya timu yenye uzoefu zaidi Bayern Munich katika Uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena usiku wa Jumatano.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Chelsea kucheza Ligi ya Mabingwa tangu Aprili 2023 na mechi hiyo ilifichua madhaifu ya timu hiyo ambayo itahitaji kutafakari ni nini kinahitajika ili kufanikiwa.
Lakini kocha mkuu Maresca anaona timu yake inaweza kujifunza mengi kutoka kwenye kipigo hicho dhidi ya Bayern na kujenga kitu huku Palmer akitupilia mbali maneno kwamba hawawezi kufanya hivyo haraka.
“Hatujaja hapa kujifunza. Tumeonesha usiku wa leo (jana jumatano) tunataka kushindana na tunataka kufanya vizuri kadri tuwezavyo,” – mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alisema.
Chelsea ilishinda Kombe la Dunia la Klabu mwezi Julai, mbele ya Paris St-Germain jijini New Jersey nchini Marekani, baada ya kushinda Conference League miezi miwili kabla.
The post “Hatujaja UCL kujifunza” – Palmer first appeared on SpotiLEO.