MANCHESTER: MSHAMBULIAJI wa SSC Napoli Rasmus Hojlund amesema hakutegemea kuzoea haraka maisha mapya ndani ya klabu hiyo na Ligi ya Italia Serie A na kufanya vizuri kiasi cha kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita.
Hojlund amesema mazingira yaliyompeleka Napoli hayakuwa sawa na wachezaji wengine ambao huhama klabu kwa Fahari bali yalikuwa yale yaliyomlazimu kupambana kuonesha uwezo wake ndani ya klabu hiyo ili kuthibitisha ubora wake baada ya kuonekana kufeli ndani ya kikosi cha mashetani wekundu Manchester United.
Katika mazungumzo na TNT Sports amesema hana chuki na yeyote klabuni hapo na jiji la Manchester ni kama nyumbani kwake kwa sababu familia yake bado ipo hapo, moyo na akili yake siku zote itakuwa jijini hapo.
“Sikutegemea, sikuzote nimejijenga kiakili, maadili yangu ya kazi kuhakikisha naongezeka kiwango kila siku. Nimepambana sana na nimekuwa na uwezo wa kushambulia sana kitu ambacho nafurahia sana kufanya. Kwahiyo ndio, ulikuwa mwaka mzuri sana, ni mwaka ambao sitausahau”
“Najua wanasoka wakubwa, wanataaluma wa taaluma zote, mchezo wowote huwa wanabaki kwenye ubora wao, kwahiyo kwangu nitaendelea kufanya nilichofanya msimu uliopita” – amesema Hojlund.
Ikumbukwe klabu hiyo ilimsajili Mdenmark Hojlund mwenye umri wa miaka 22 kwa mkataba wa mkopo kutoka Manchester United wenye kipengele cha kumnunua kwa Euro milioni 44. Msimu uliopita, Rasmus alifunga mabao 10 na kutoa asisti 2 katika mechi 52.
The post “Sikutegemea kufanya makubwa Napoli” – Hojlund first appeared on SpotiLEO.