BARCELONA: MABINGWA wa LaLiga FC Barcelona wamethibitisha kuwa mechi yao ijayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG) itachezwa kwenye Uwanja wa Lluís Companys Olympic Stadium, kutokana na kutokamilika kwa ukarabati wa uwanja wao wa Camp Nou.
Barcelona walikuwa na matumaini ya kurejea Camp Nou mpya iliyofanyiwa ukarabati mwanzoni mwa msimu huu, lakini ucheleweshaji wa ujenzi umeilazimisha klabu hiyo kuendelea kucheza mechi zake za nyumbani nje ya dimba hilo
Klabu hiyo imeamua kuwa itawakaribisha PSG kwenye Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 55,000 baada ya kulazimika kucheza na Valencia katika mchezo wake wa kwanza wa nyumbani wa LaLiga msimu huu kwenye uwanja wao mdogo wa Estadi Johan Cruyff, ambao unachukua watu 6,000 pekee ukiwa nje ya jiji hilo.
Barcelona pia itacheza na Getafe Jumapili kwenye uwanja wa huo huo, ambao kwa kawaida hutumiwa na timu yake ya wanawake.
Mabingwa wa Ulaya PSG watakuwa Barcelona katika siku ya kwanza ya mwezi Oktoba kwenye mzunguko wa pili wa mechi za ligi ya Ligi ya Mabingwa.
Barcelona imesema katika taarifa kwamba inafanyia kazi upatikanaji wa vibali muhimu kutoka kwenye mamlaka kwa ajili ya ufunguzi wa Spotify Camp Nou katika miezi ijayo
The post “Barcelona Vs PSG hakipigwi Spotify Camp Nou” first appeared on SpotiLEO.