Taarifa kwa Umma kutoka klabu ya Simba SC juu ya Kocha wa Muda wa klabu hiyo.
Klabu ya Simba inamtangaza, Hemed Suleiman maarufu Morocco kuwa Kocha wa muda ‘Caretaker wa Klabu yetu kwenye mechi za Kimataifa baada ya Kocha, Fadlu Davids kusitisha mkataba na Kocha Selemani Matola kuwa na kadi nyekundu.
Uongozi wa klabu unalishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco ambae ni Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania kujiunga nasi katika kipindi hiki ambacho Klabu inakamilisha taratibu na mchakato wa Kocha wa kudumu wa Klabu yetu.
Kocha Morocco ataliongoza benchi la ufundi kuelekea Mchezo wa Marudi-ano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United FC Septemba 28, 2025.
Imetolewa na:
Uongozi Klabu ya Simba 22 Septemba, 2025.