Nyota wa Barcelona raia wa Hispania na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kijana kwa msimu wa pili mfululizo Lamine Yamal amempongeza mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or usiku wa jana Ousmane Dembele kwa kufanikiwa kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Dunia 2025.
Lamine ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiandika ujumbe wa shukrani kwa tuzo aliyoitwaa mara ya pili huku akiambatanisha na pongezi hizo kwa staa huyo wa PSG.
“Mpango wa Mungu ni Mkamilifu na ni lazima upande ili kufika kileleni,Nimefurahia kushinda tuzo ya Kop mara ya pili na nampongeza Ousmane Dembele kwa tuzo hiyo na msimu mzuri”Ameandika Lamine.