DAR ES SALAAM: MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Yanga leo saa 1:00 usiku wanashuka dimbani kuikabili Pamba katika mchezo wa kwanza msimu wa 2025/2026 utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Yanga imetoka kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete ya Angola kwa ushindi wa mabao 3-0.
Wananatarajiwa kuendeleza morali waliyoonesha katika mchezo huo wa kimataifa ingawa huenda wakakutana na upinzani wa Pamba kutegemea na walivyojipanga.
Pamba imeshacheza mchezo mmoja wa ligi dhidi ya Namungo ambapo walitoka sare ya bao 1-1.
Timu hizo mara ya mwisho zilikutana msimu uliopita ambapo Yanga iliondoka na pointi sita. Mchezo wa kwanza walishinda mabao 4-0 Oktoba mwaka jana kish awa pili walikutana Februari mwaka huu na Yanga kushinda 3-0.
Mchezo huo wa ligi utakuwa ni mtihani wa kwanza wa Kocha mpya wa Yanga Romain Folz ambaye ataanza kuonja ladha Pamoja na baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.
Ubora wa kikosi cha Yanga msimu huu huenda ukawabeba lakini mwisho wa yote ni dakika 90 za mchezo utaamua nani zaidi.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu utakaochezwa ni Azam FC dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Ni mchezo chini ya Kocha mpya Florent Ibenge na wachezaji baadhi wapya watakaotizamwa.
Azam imetoka kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Merrikh ya Sudan mabao 2-0 hivyo, inategemewa kwa ubora ule ule iliouonesha basi itaendeleza kwenye ligi.
Mbeya City wamerejea Ligi Kuu msimu huu baada ya kushuka mwaka jana. Na tayari wametoka kushinda mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Fountain Gate bao 1-0.
Miaka ya nyuma ilikuwa ni timu inayoleta ushindani. Dakika 90 za mchezo wa leo utakaochezwa saa 3:00 usiku zitaonesha nani zaidi.
The post Yanga, Azam FC kuzichanga karata leo first appeared on SpotiLEO.