BARCELONA: MABINGWA wa LaLiga FC Barcelona wamethibitisha kuwa Kiungo wa kati wa klabu hiyo Gavi atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kinachofika hadi miezi mitano baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti kutibu jeraha la meniscus,
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 21, aliumia goti lake la kulia mazoezini mapema mwezi Agosti baada ya kucheza mechi mbili tu za ufunguzi za Barca msimu huu.
“Gavi amefanyiwa upasuaji na kushonwa ili kutatua tatizo lake la jeraha la ‘meniscus’. Muda wa kupona unakadiriwa kuwa miezi minne hadi mitano,” Barca imesema katika taarifa Jumanne usiku.
Barca wanashika nafasi ya pili kwenye LaLiga, wakiwa nyuma ya Real Madrid kwa pointi tano lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi, wakitarajiwa kuwa wageni wa Real Oviedo kesho alhamisi.
The post Gavi ‘ndo’ mpaka mwakani first appeared on SpotiLEO.