Gwiji wa Manchester United Wayne Rooney hajawahi kuona haya kueleza hisia zake.
Mchezaji huyo wa zamani na kocha bado anaamini kuwa Lionel Messi ndiye mchezaji bora zaidi kuliko Cristiano Ronaldo huku akisisitiza kwamba hamchukii fowadi huyo anayekipiga na klabu ya Al Nassr.
Akiongea kwenye podcast ya Rio Ferdinand Rooney alisema;
“Watu wanadhani namchukia! Nampenda! Ni mkali sana na anafanya maajabu. Sidhani kama watu wanatambua jinsi mimi na yeye tulivyokuwa karibu.”
“Mimi napendelea jinsi Messi anavyocheza, ndio hivyo, wewe unaweza kumpenda Cristiano na mwingine akampenda Messi” akamalizia Rooney.