Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wake, Auka Gecheo mara moja.
Inafahamika kuwa Kamati ya Utendaji, ikiongozwa na Kaimu Rais Alexandre Muyenge, iliyokutana takriban tarehe 18 mwezi huu, iliazimia kwa kauli moja kumsimamisha Auka katika nafasi yake ya Mkurugenzi Mtendaji.
CECAFA EXCO, hata hivyo, haikufichua sababu ya hatua hiyo, lakini inaeleweka Mkenya mwingine anatazamiwa kuchukua jukumu hilo.
Auka amehudumu katika nafasi hiyo tangu kuteuliwa kwake Julai 2020, alipochukua nafasi ya Nicholas Musonye, aliyekuwa Katibu Mkuu.