Manchester United inamtaka mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 32, ambaye huenda akaondoka Bayern Munich msimu ujao wa kiangazi.
Tetesi zinaonyesha kwamba nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur anaweza kutaka kumalizia kibarua chake Allianz Arena msimu ujao wa joto, licha ya kuongezewa kandarasi hadi 2027.
Kulingana na gazeti la Daily Star, “Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anaripotiwa kuwa na hamu ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza baada ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, huku Manchester United ikitajwa kuwa timu inayohitaji kwa ukubwa huduma ya mchezaji huyo.
Taarifa zinasema Kane ataweza kupatikana kwa ada ya pauni milioni 56.8.