DAR ES SALAAM: SHIRIKISHO la Ngumi Tanzania (BFT) limechagua mabondia 26 na jopo la ufundi la watu tisa kwa ajili ya kuanza mazoezi kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kanda ya tatu Afrika yatakayofanyika Nairobi Kenya Oktoba 14 hadi 15, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga leo kikosi hicho kimeteuliwa baada ya mashindano ya Klabu bingwa ya Taifa yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Tanga.
“Kikosi kiko tayari kuinua bendera ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa. Mashindano ya Nairobi Kenya yatatumika kama jaribio la kwanza la kimataifa kwa maandalizi ya michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 yatakayofanyika Glasgow, Scotland Julai 23 hadi 2 Agosti 2026, ambayo shirikisho pia linajiandaa kushiriki,”ilisema taarifa hiyo.
Mabondia wanaume waliochaguliwa ni Juma Athumani- MMJKT, Azizi Chala- Ngome, Faki Issa – Jeba Tanga, George Costantino- Ngome, Ezra Paulo- Ngome, King Lucas- Ngome, Rashid Mrema – Polisi, Abdallah Mfaume- Ngome, Khasim Mbundwike Ngome, Ezi Kasililika – Magereza na Joseph Sylevester MMJKT.
Wengine ni Yusuf Changalawe- Ngome, Alfonce Abel- MMJKT, Mussa Malegesi Ngome, Agostino Chilungwana – MMJKT na Maximillian Patrick – MMJKT.
Kwa upande wa wanawake, Martha Kimaro- Ngome, Aisha Hamisi JKT, Sarafina Fusi Ngome, Zulfa Macho Ngome, Zawadi Kutaka JKT, Vumilia Kalinga Ngome, Salma Yahaya Magereza, Salma Changarawe Kigamboni, Recho Msengi Dodoma, Veronica Ebroni Magereza.
Viongozi wa ufundi ni Samwel Kapungu – Mwalimu Mkuu BFT, Mzonge Hassani- Mwalimu msaidiza Ngome, Muhsini Mng’ola – Mwalimu- MMJKT, Geradi Betweli- Mwalimu- Ngome, Khasimu Abdallah – Mwalimu- MMJKT.
Wengine ni Doto Kasongo- Mwalimu- Ngome, Fatuma Manzi, Said Hofu Mwamuzi MMJKT, Baraka Jeremani Mwamuzi Polisi na Mussa Magolima Daktari.
The post Mabondia 26 kushiriki mashindano kanda ya tatu first appeared on SpotiLEO.