MANCHESTER: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amemtaja beki wa zamani wa klabu hiyo Kyle Walker kama mmoja wa mabeki wa pembeni bora zaidi wa muda wote na kumweka katika mizani sawa na nyota kama Cafu na Javier Zanetti kabla ya kwa beki huyo wakimataifa wa England kurejea Etihad akiwa na Burnley Jumamosi.
Itakuwa ni mechi ya kwanza kwa Walker mwenye umri wa miaka 35 dhidi ya kabu yake ya zamani Man City tangu aondoke katika klabu hiyo aliyoitumikia kwa miaka nane, baadhi akiwa kama nahodha. Alitumia sehemu ya msimu uliopita akiwa mkopo AC Milan kabla ya kuhamia Burnley iliyopanda daraja msimu huu.
“Bila shaka,” Guardiola alijibu, alipoulizwa kama Walker anastahili kutajwa sambamba na mabeki wa kulia bora duniani kama vile mchezaji wa zamani wa Brazil Cafu, beki wa zamani wa Argentina Zanetti na nyota wa Ufaransa Lilian Thuram. “
“Walker ni moja ya mabeki wa pembeni bora zaidi wa muda wote. Ukihitaji kuudhibiti upande huo, nilikuwa nalala vizuri kabla ya mechi Kyle akiwa eneo hilo. Anaweza kushughulika na mawinga wa kiwango cha juu kabisa duniani kwa kasi yake.” – alisema Pep
Walker alishinda mataji sita ya Premier League na moja la Champions League akiwa Man City, Pamoja na maataji mengine sita ya ndani kabla ya kiwango chake kuonekana kushuka msimu uliopita na kupoteza namba ndani ya kikosi cha Guardiola
The post Pep amuweka Walker meza moja na Cafu, Zanetti first appeared on SpotiLEO.