Romain Folz mpaka sasa chumba chake cha kubadilishia nguo kitakuwa na amani na ushindani ambao una afya kwa ajili ya mafanikio ya timu.
Amezungumza kuwa kila mchezaji atapewa nafasi na kila mechi tutegemee kuona sura tofauti, hali inafanya kila mchezaji ajione ana nafasi ya kufanya vizuri wachezaji kama Edmund John watakuwa wanaona hatukosea kuja Yanga SC.
Mchezaji binafsi anapenda kuona anapewa majukumu na usawa kwenye kikosi unafanya kila mmoja awe na heshima kwa mwenzake moja ya jambo ambalo litafanya Folz afanikiwe kama atakaa kwa muda mrefu Yanga SC basi ni Man Management kusimamia wachezaji na kufanya wote wawe na furaha jambo huwa ni ngumu.
Kauli ya leo ni habari nzuri kwa wachezaji wote wa Yanga SC na nadhani ikiwa hivyo basi wataendelea kuzichapa timu.
.”Kwangu mimi kila mchezaji ni muhimu kwenye timu, najua kupanga wachezaji wale wale kila siku kuna namna unawavunja moyo wachezaji wengine kwahiyo hata kesho tegemeeni mabadiliko”
“Nafahamu kuna wakati tutapaswa kuwa bora zaidi ya sasa, tutatakiwa kuwa kwenye ubora wa hali ya juu hicho kipindi kitafika lakini sio sasa “
“Kwa sasa tutaendelea kufanya mabadiliko lakini kipindi kitafika tutakuwa tofauti kabisa na mnavyotutazama sasa”
– Kocha wa Yanga