Mara baada ya kocha mkuu wa Yangasc Romain Folz kuwa na kiwango ambacho sio cha kuridhisha kwenye michezo kadha ambayo ameisimamia klabu hiyo hatimaye uongozi wa Yangasc umeanza mchakato wa kutafuta mwalimu mpya ambaye atakuja kurithi mikoba ya mfaransa huyo
Na majina ambayo yanatajwa kwa ukubwa kikosini humo ni aliyekuwa kocha mkuu wa zamani wa klabu hiyo Nasreddine Nabi ambaye kwa sasa yupo nchini Tanzania
Lakini mara baada ya tetesi hizo Kasaco media ilimtafuta kocha huyo hili kuja ukweli wa taarifa
Nabi alisema “Nimeona watu wanasema nimekuja hapa kwa ajili ya Simba, wengine wanasema Yanga, hapana! Nipo hapa kwa safari yangu binafsi, nadhani hii ni mara ya tatu nakuja hapa,
“Tanzania ni nyumbani ndio maana napenda sana kuja hapa, tangu nimefika sijakutana na kiongozi yeyote wa Simba wala Yanga, nikimaliza mambo yangu nitaondoka.” ALISEMA NABI
Lakini pia jina lengine ambalo lipo mezani kwa Yangasc ni la kocha mkuu wa kikosi cha Gaborone United ya nchini Botswana ambaye siku chache alikuwa nchini akikiongoza kikosi hicho kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika mbele ya kikosi cha simbasc Dimitar Pantev raia wa Ubelgiji
Mpaka hivi sasa uongozi wa Yangasc aujatoa taarifa yeyote kuhusu hatima ya Romain Folz lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa uongozi wanataka kuutumia muda wa international black kupisha kalenda ya fifa mwalimu mpya kuandaa kikosi hicho .