DAR ES SALAAM:MSANII maarufu wa filamu za Bongo Movie, Kajala Masanja, ameweka wazi kuwa amekata tamaa ya kuzaa mtoto mwingine kutokana na umri wake na changamoto alizowahi kukutana nazo huko nyuma katika harakati za kutaka kupata mtoto wa pili.
Kajala amesema kuwa kwa kipindi cha nyuma alikuwa akitamani sana kuongeza mtoto, lakini juhudi hizo hazikufanikiwa, na sasa umri umesogea hivyo ameona ni bora kuangazia mambo mengine muhimu katika maisha yake.
“Nilitamani sana kupata hata watoto wawili, lakini ilishindikana kwa wakati. Hivyo nimeona bora sasa kuangalia kitu kingine mbele maana nimekata tamaa kabisa ya kuongeza mtoto mwingine. Ninajikita kwenye kumuwezesha Paula asonge mbele kielimu,” amesema Kajala.
Msanii huyo, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 43, amesema anaona tayari ameshakuwa mtu mzima na anataka kutumia muda wake kufanya mambo yatakayompa tija zaidi maishani.
Kajala ana mtoto mmoja aitwaye Paula, ambaye alizaa na mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, P-Funk Majani.
The post Kajala asema amekata tamaa ya kuzaa tena first appeared on SpotiLEO.