MAREKANI:MTANZANIA anayekuja kwa kasi katika anga la biashara za kimataifa, Vincent Kiango, ameibuka gumzo nchini Marekani baada ya kutambulisha kinywaji kipya cha maji safi ya kunywa chenye chapa Safari Black Mineral Water.
Bidhaa hiyo imekuwa kivutio kikubwa sokoni kutokana na ubora wake, ladha tamu, na muonekano wa kifungashio chake, hali iliyosababisha ianze kushindana kwa kasi na chapa nyingine maarufu za maji baridi nchini humo.
Kiango amesema kuwa Safari Black Mineral Water ni maji bora yanayozingatia viwango vya afya, tofauti na baadhi ya maji mengine ambayo hutumia kemikali za kuhifadhia chakula.“Wateja wanahitaji maji yanayojali afya zao.
Safari Black Mineral Water ni bidhaa mpya Marekani lakini inapendwa na wengi, hasa wazungu ambao wanajali afya zao. Tumetengeneza chupa zinazobebeka kirahisi, zina mvuto, na maji haya yanakata kiu bila madhara kwa mnywaji,” amesema Kiango.
Aliongeza kuwa bidhaa hiyo kwa sasa inapatikana nchini Marekani na imeanza kusambazwa kimataifa, ikipatikana kwa njia ya mtandao kupitia Amazon.
Aidha, wafanyabiashara wa vinywaji baridi wanaotaka kuweka oda au kushirikiana kibiashara wametakiwa kutembelea tovuti yao rasmi www.safariblackwater.com ili kujipatia kinywaji hicho kipya kinachopata umaarufu mkubwa duniani.
The post Safari Black Mineral Water gumzo Marekani first appeared on SpotiLEO.