Mchambuzi nguli nchini Dominic Salamba amesema Klabu ya Simba ingekua na kikosi angalau kama ilivyo Yanga,Azam na hata Singida Black Stars wangekua na uwezo wa kutwaa Ubingwa wa Afrika.
Salamba amesema Simba Sc ni Klabu ambayo inauwezo wa kuyacheza vizuri mashindano ya kimataifa licha ya upungufu walionao kwenye kikosi chao.
Mchambuzi huyo ameimwagia sifa kem kem Simba Sc akiweka wazi ya kwamba Simba hii licha ya kuwa na Meneja mpya ndani ya wiki mbili tu lakini waneonesha ukomavu mkubwa,wakaweza kuhimili presha wakiwa ugenini napia wakawa bora kwenye matumizi ya nafasi walizopata jambo ambalo si rahisi kama wengi walivyofikiria.
“Ubora wa vikosi vya Yanga,Azam na Singida Black Stars ndio ungehamishiwa katika Klabu ya Simba nina hakika mnyama angeweza kutwaa wa Afrika”
By Dominick Salamba