NAIROBI: TAMASHA la Filamu la Nairobi (NBO Film Festival) Toleo la 7 limepangwa kufanyika kuanzia Oktoba 15 hadi 25 mwakani jiji la Nairobi nchini Kenya.
Tamasha hilo linalosherehekea uandishi wa hadithi za Kiafrika na Mahusiano ya Kidunia toleo la 6 lilihitimishwa kwa mafanikio katika kituo cha Prestige Cinema, Ukumbi wa Kaloleni Social Hall, Nairobi, baada ya siku 10 za maadhimisho ya filamu, ubunifu, mijadala, na uandishi wa hadithi za Kiafrika huku zaidi ya filamu 26 kutoka nchi zaidi ya 15, zikiwemo filamu mpya zilizozinduliwa duniani kwa mara ya kwanza, filamu za Afrika, pamoja na filamu zilizopata sifa kimataifa.
Jopo la majaji la NBO Film Festival 2025 lilimkabidhi Tuzo Kuu ya Majaji (Grand Jury Prize) kwa filamu My Father’s Shadow ya Akinola Davies kutoka Nigeria filamu ya kwanza kutoka nchini humo kuwahi kuchaguliwa kuonyeshwa katika Tamasha la Filamu la Cannes.
Pia, majaji walitoa Tuzo Maalum (Special Mention) kwa filamu The Dog, filamu ya uhalifu ya kusisimua na yenye ujumbe mzito, iliyothibitisha uwezo mkubwa wa sekta ya filamu barani Afrika.
“Tulivutiwa sana na ubora na utofauti wa filamu zilizoshiriki mwaka huu. Tuliamua kwa pamoja kuipa heshima filamu iliyotugusa kwa undani hadithi ya hisia kuhusu upendo wa kifamilia, hamu ya kukutana tena na baba, na matumaini ya mabadiliko katika jamii ya Nigeria. ‘My Father’s Shadow’ inaangazia kwa ustadi uhusiano wa baba na mwana kwa upole na udhaifu wa kibinadamu, ikinasa hisia za kizazi kinachotafuta tumaini jipya.”
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017, NBO Film Festival imekua na nguzo muhimu ya utamaduni Afrika Mashariki, ikitoa nafasi kwa sauti za waandishi wa Kiafrika na kuonesha nguvu ya filamu kama nguvu ya kuunganisha na kubadilisha jamii.
The post Tamasha la 7 la filamu la NBO Kenya kufanyika Oktoba 15, 2026 first appeared on SpotiLEO.






