NAIROBI: WAPENZI mashuhuri Andrew Smollo na Boera Bisieri wako mbioni kuandika historia mpya wanapojiandaa kuigiza pamoja kwa mara ya kwanza katika jukwaa la Kenya National Theatre.
Hili ndilo onesho lao la kwanza la wawili hao jukwaani tangu waanze safari yao ya sanaa na mapenzi.
Onesho hilo, la ‘The Vows’, ni mchanganyiko wa hisia halisi, vicheko, uchungu na utamu wa mahusiano ya kibinadamu.
Watazamaji wanatarajiwa kuingia kwenye safari ya hisia kutoka kwa wasanii hao kufurahia onesho hilo na kuburudika kwa watakachokionesha kwao.
“Mimi na mume wangu tutakuwa jukwaani peke yetu kwa mara ya kwanza! Nimeingiwa na uoga, lakini nina msisimko usioelezeka,” Bisieri alifichua. “Hii ni hadithi ya mapenzi yenye mtiririko mzuri wenye hisia za upendo, vichekesho, maumivu na uhalisia wa mahusiano ya kisasa.”
Mkurugenzi wa onesho hilo, Ben Tekee, ambaye amekuwa mwongozaji maarufu katika tasnia, anasema mradi huu unamgusa kwa namna ya kipekee.
“Baadhi ya hadithi ni nzuri mno kiasi kwamba haziwezi kubaki bila kusimuliwa… na hii ni maalum zaidi kwangu,” alieleza. “Nimebahatika kushuhudia safari ya mapenzi ya wanandoa hawa, na hata kuchangia kuwaunganisha.
Onesho hili linatarajiwa kuvutia mashabiki wa sanaa na wapenzi wa hadithi zenye uhalisia wa maisha, na bila shaka litafungua ukurasa mpya katika safari ya wanandoa hawa wenye vipaji vya kipekee.
The post Wapenzi wachekeshaji kufanya Onesho lao la kwanza first appeared on SpotiLEO.




