MILAN: KOCHA wa zamani wa SSC Napoli, Luciano Spalletti anatarajia kurejea jijini Napoli Jumapili kwa mara ya kwanza tangu aiwezeshe klabu hiyo kutwaa taji lake la kwanza la Serie A baada ya zaidi ya miaka 30.
Spalletti amesema tayari anahisia kali kuhusu kurejea huko. Safari hii akirejea si tena kama rafiki na mkufunzi wa kikosi hicho bali kama kocha wa timu pinzani ya Juventus.
“Kutakuwa na hisia kali kwa sababu nina marafiki wengi wanaonisubiri pale. Haijalishi nitapokelewa vipi, lakini hisia nilizo nazo kwao ni zile za mtu anayewapenda sana.”- Spalletti amesema.

Spalletti aliondoka Napoli mwaka 2023 baada ya kuitwalia taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33, akisema wakati huo kwamba alihitaji mwaka mmoja wa mapumziko. Hata hivyo, miezi mitatu baadaye aliteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia baada ya Roberto Mancini kujiuzulu ghafla.
Spalletti alitimuliwa kwenye majukumu ya Italia mwezi Juni na baadaye Oktoba Juventus ikamwajiri baada ya Bianconeri kumfukuza Igor Tudor kufuatia mwanzo mbaya wa msimu.
Juventus inashika nafasi ya saba kwenye Serie A lakini iko nyuma kwa pointi tano tu dhidi ya vinara wenza Napoli na AC Milan. Haijashinda Serie A tangu 2020 ilipomaliza ubabe wa mataji tisa mfululizo, enzi ambayo ilianzishwa na Antonio Conte, ambaye sasa ndiye kocha wa Napoli.
The post Spalletti ajawa hisia mesto Napoli first appeared on SpotiLEO.






