“Najua madaraka ni matamu sana,najua mtu yuko tayari kufa ila siyo kuachia madaraka hususa ni pale anapoonja utamu wa pesa ya madaraka…..siyo dhambi kubaki madarakani ila hakikisha unawapa raha mashabiki wako”
“Siku zinazidi kusonga,Simba wametawaliwa na Yanga kwa miaka minne na wala hakuna dalili ya kuvunja uteja leo wala kesho”
“Viongozi wa Simba wameshindwa kujenga timu ya maana ili kuwapiku Yanga,wamefanya usajili wa wachezaji zaidi ya 120 kwenye madirisha 9 yaliyopita ila ngoma bado ni ngumu”
“Kinachofanyika baada ya mashabiki kupiga kelele ni kubadilishana vyeo,C.E.O atakuwa Mwenyekiti wa Bodi,kisha mwenyekiti wa bodi atakuwa Rais wa heshima”
“Kinachobadilika ni vyeo ila watendaji ni wale wale,akili ni zile zile ambazo zimefeli miaka nenda rudi……hakuna jipya”
“Mimi nadhani Kama hawa viongozi wamegoma kuondoka Simba basi wakubali kuajiri hawa watu wawili (Mkurugenzi wa michezo na mkurugenzi wa ufundi)kisha wawape uhuru wa kusajili na kutengeneza Simba mpya”
“Mkurugenzi wa ufundi anaweza kuibeba project ya timu kuanzia usajili wa wachezaji hadi kocha kisha akarudisha heshima msimbazi ila kwa hawa wa sasa Sioni dalili leo wala kesho🙌”
The post Hans Raphael “Viongozi wa Simba Wameshindwa Kujenga Timu” appeared first on SOKA TANZANIA.






