MUMBAI: Sunny Deol ambaye ni mtoto wa muigizaji wa filamu kutoka India aliyefariki dunia hivi karibuni Dharmendra amechapisha ujumbe wa kumkumbuka baba yake ikiwa ni siku kadhaa tangu kifo chake. Dharmendra aliaga dunia mnamo Novemba 24 mwaka huu, siku chache tu kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 90, Desemba 8.
Sunny akimkumbuka baba yake, alishiriki video yao ya zamani akiwa naye na aliambatanisha na ujumbe wenye hisia kali.
Video hiyo inaonesha Sunny na Dharmendra wakiwa likizo milimani. Sunny akirekodi Dharmendra akizama katika uzuri wa milima huku akionekana kurukaruka akiwa amevalia koti jeusi na kofia. Tunasikia sauti ya Sunny ikirekodi video ikimuuliza Dharmendra, “Kwa hivyo Papa unafurahia?” Dharmendra akatoa kicheko na kusema, “Ninafurahia sana mwanangu, inapendeza.” Sunny alionesha milima na kusema, “Ni nzuri.”
Kwa kunukuu, Sunny Deol aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa Kihindi na kusema, “Leo ni siku ya kuzaliwa ya baba yangu. Papa yuko nami kila wakati, ndani yangu, nakupenda papa. Miss you.” Hii ni mara ya kwanza Sunny ameshiriki chapisho karibu na Dharmendra tangu kifo chake. Hapo awali, mwigizaji huyo alionekana kukasirishwa na paparazzi wakati Dharmendra alilazwa hospitalini na kuomba faragha kwa familia yake. Tangu kifo cha Dharmendra, familia ya Deol imedumisha umbali kutoka kwa vyombo vya habari.
Mapema leo, Esha Deol pia alikuwa amemkumbuka Dharmendra na kuandika jinsi anamkumbuka sana baba yake. Aliandika, “Kwa Baba yangu kipenzi mkataba wetu, ni dhamana kubwa zaidi, sisi katika maisha yetu yote, ulimwengu wote na zaidi siku zote tuko pamoja baba, iwe mbinguni au duniani. Sisi ni wamoja mpaka sasa umekuwepo moyoni mwangu kwa upole, kwa uangalifu na kwa thamani kabisa ili kuendelea nami katika somo hili la thamani kwa maisha yote kumbukumbu zote za maisha mafundisho, mwongozo, uchangamfu, upendo usio na masharti, heshima na nguvu uliyonipa kama binti yako haiwezi kubadilishwa au kulinganishwa na mtu yeyote.”
Aliongezea”Ninaahidi kuendeleza urithi wako na kueneza fahari yako kwa milioni ya watu waliokupenda kama nlivyokupenda nakupenda baba binti yako kipenzi , Esha wako , Bittu wako.”
Dharmendra alikuwa na wake wawili. Mke wake wa kwanza anaitwa Prakash Kaur na kubarikiwa watoto wanne anbaye ni Sunny Deol, Bobby Deol, Ajeita Deol na Vijeta Deol. Lakini pia Dharmendra alikuwa na mke wa pili pia anayeitwa Hema Malini na kubahatika kupata mabinti wawili Esha Deol na Ahana Deol.
The post Sunny Deol amkumbuka baba yake, aachia ujumbe first appeared on SpotiLEO.




