Afisa habari wa klabu ya Simba Sc Ahmed Ally amefunguka mambo mazito kuhusiana na tetesi za winga hatari wa klabu hiyo Ellie Mpanzu kuhitajika na watani wao wa jadi yaani klabu ya Yanga Sc.
Ahmed Ally katika taarifa yake aliyoitoa siku ya leo Alhamisi December 18 kupitia Efm Tanzania amethibitisha kwamba siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi nyingi sana ambazo zinadokeza kwamba Yanga Sc wamefanya mazungumzo ya awali na Ellie Mpanzu.
Ahmed Ally katika taarifa yake ameendelea kueleza kwamba tetesi hizo hazina ukweli wa aina yoyote bali ni taarifa ambazo zimeibuliwa kwa lengo la kupeleka presha kwenye timu yao haswa katika wakati huu ambapo timu haifanyi vizuri kwenye michuano ya ndani pamoja na ile kimataifa.
Ahmed Ally ameeleza wazi kwamba Ellie Mpanzu bado amebakiza mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kuwatumikia Simba Sc na wala hawezi kusaini Yanga Sc kama inavyozushwa na baadhi ya watu wachache wenye nia mbaya na maendeleo ya klabu ya Simba Sc.
Ahmed Ally amemaliza utata wa sakata hili kwa kueleza kwamba Ellie Mpanzu ameridhia kuendelea kuwatumikia Simba Sc kwa muda mrefu na wala hajawai kuonyesha dalili zozote za kutaka kuondoka katika klabu hii kubwa na kongwe kwenye historia ya soka la Tanzania bara.
Taarifa hii kutoka kwa Ahmed Ally imekuwa njema sana kwa mashabiki na wadau wa klabu ya Simba Sc ambao walianza kupata wasiwasi juu ya hatma ya winga huyu ambaye amekuwa akitolewa macho sana na watani wao wa jadi yaani Yanga Sc.
Taarifa hii imekuwa mbaya zaidi kwa mashabiki na wadau wa klabu ya Yanga Sc ambao walikuwa wanaamini kwamba Mpanzu atajiunga na timu yao hivi karibuni kutokana na tetesi za kwenye mitandao ya kijamii.
Sports_HQ
The post Ahmed Ally Afunguka Dili la Elie Mpanzu Kwenda Yanga appeared first on SOKA TANZANIA.







