Raia wa Msumbiji walianza mapema asubuhi siku ya Jumatano kupiga kura siku kumchagua rais wao na bunge. Upinzani unasema unahofu na wizi wa kura.
Takribani wapiga kura milioni 17 katika taifa hilo lenye watu milioni 31, wamejiandikisha kupiga kura kumchagua rais ajaye, pamoja na wabunge 250 na magavana wa majimbo.
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za Msumbiji na vitafungwa saa 12 jioni. Wagombea wanne wanashindana katika uchaguzi huo kuchukua nafasi ya Rais Filipe Nyusi, ambaye amemaliza muda wake wa mihula miwili kwa mujibu wa katiba.
Rais anayemaliza muda wake, Filipe Nyusi, alikuwa mmoja wa wa kwanza kupiga kura katika kitongoji tajiri cha Maputo.
Ametoa wito wa uchaguzi wenye “tulivu na amani”, akiomba kusiwepo na “kundi linalojisifu au kutishia wengine” na kwamba kila mtu “aepuke kutangaza matokeo yamapema.
Uchaguzi wa 2019, ambao ulitoa 73% ya kura kwa mgombea wa chama cha FRELIMO ulikumbwa na kasoro na uchaguzi wa mitaa wa mwaka jana ulipingwa vikali na upinzani.
The post Wamsumbiji wapiga kura katika uchaguzi mkuu wenye ushindani mkubwa first appeared on Millard Ayo.