KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi taifa (CCM- NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla ameupongeza Mkoa wa Dar es salaam kwa kutoa ushirikiano nakufikisha asilimia 96.7 katika zoezi la uandiskishaji wa daftari la wakazi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.
CPA Makalla ametoa pongezi hizo leo Oktoba 22,2024 katika mkutano uliofanya kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es salaam akiwa na viongozi wa chama wa mkoa huo na waandishi wa habari.
Aidha, amesema Dar es salaam ni mkoa wenye idadi kubwa ya watu ambao ndio wapiga kura, hivyo jambo hilo ni faraja kubwa kwa CCM. Pia alipongeza kazi kubwa yenye kuzaa matunda iliyofanywa na viongozi wa ngazi zote kutoa elimu na uhamasishaji juu ya umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura.
“ Hiyo maana yake Dar es salaam kwa ukubwa wake kwa idadi kubwa ya watu kuweza kufika asilimia hii asilimia 96.7 inaonesha namna walivyo na muamko wa kuchagua viongozi,” amesema Makalla
The post CPA Makalla aupongeza Mkoa wa Dar kwa kwa kufikisha asilimia 96.7 katika zoezi la uandiskishaji daftari la wapiga kura first appeared on Millard Ayo.