Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema bidhaa nyingi za vyakula vinavyofungashwaΒ na visivyokidhi vigezo vya usalama na ubora ,vimekuwa vikikataliwa kusajiliwa na kutoruhusiwa kuingizwa nchini.
Kwa uzuiaji wa bidhaa hizo,TBS imeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kulinda na kuendeleza afyaΒ ya jamii na soko la Tanzania dhidi ya bidhaa za chakula zisizo na usalama na ubora.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, David Ndibalema, wakati wa Mkutano wa TBS na waingizaji wa vyakula nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Dibalema alisema tangu TBS ipewe jukumu la kusimamia sheria ya usalama wa chakula nchini, kwa kutumia dirisha la usajili katika kumlinda na kuendeleza afya ya mlaji imeweza kupiga hatua mbalimbali ambazo zimeweza kuzuia bidhaa zaΒ chakula zisizo na usalama na ubora kutoingia nchini wala kusambaa sokoni.
Alisema ikumbushe kuwa usajili wa bidhaa za vyakula vilivyofungashwa ni takwaΒ la kisheria linalolenga kuhakikisha kuwa vyakula salama na bora ndivyo vinaruhusiwa kuingizwa sokoni ili kulinda na kuendeleza afya ya mlaji na jamii kwa ujumla.
Alisema usajili huo pia unasaidia kulinda na kuendeleza biasharaΒ kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa na sera za nchiΒ za kiuchumi zilizopo hasa zile zinazohusu uwezeshaji wa uwepoΒ wa mazingira mazuri ya ufanyaji biashara nchini.
βNimefurahi sana kushiriki mkutano huu wa wafanyabiashara wanaoagiza na kuingiza bidhaa za chakula kilichofunganishwa nchini,muitikio wenu ni ishara kuwa mkutanoΒ huo una umuhimu mkubwa katika kuhakikisha kuwa bidhaa zinazotengenezwa na viwanda husika ,kisha kuingizwa nchini usalama na ubora wakeΒ unafahamika kwa kutumia vigezo vya kisayansiΒ bila kukwamisha ufanyaji biashara.
βLengo kuu likiwa ni kulinda na kuendeleza afya ya mlaji pamoja na kulinda soko la Tanzania dhidi ya bidhaa za vyakula visivyo salama na bora,βalisema Ndibalema.
Alisema mkutano huo utatoa fursa kupata uelewa wa pamoja ili shughuli za kusimamia salama wa chakula nchini ziweze kuwa ni zenye ufanisi kupitia nguvu ya pamoja baina ya wafanyabiashara, walaji na wasimamizi.
Aidha NdibalemaΒ alisema matarajio ya shirika lao kupitia mkutano huo utasaidia kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbaliΒ kutoka kila upande ikiwemo mwingizaji bidhaa kufahamu sababu zianzopelekea wakati mwingine bidhaa yake anayotaka.kuingiza nchini.kukataliwa usajili na kujua tathimini zinazofanyika kwa bidhaa kukataliwa kusajiliwa.
Awali akimkaribisha mgeni Ndibalema, rasmi, Meneja wa Usajili wa Bidhaa na Majengo wa TBS, Habakuki Kalebo,Β alisema wamekuwa wakipokea maoni na maombi mbalimbali kutoka kwa wadau wa Shirika yanayohusu namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utendaji wao na kuboresha huduma zao kwa jamii wanayoihudumia.
βMkutano huu unatarajia kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwa na uelewa wa pamoja baina ya pande mbili hususan kwa baadhi ya maeneo ambayo wamebaini kuwa wanauelewa mdogo au tofauti baina ya pande hizo mbili,βalisema Kalebo.
Alisema moja ya mbinu ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kwa wateja na wakati huo kuongeza ufanisi wa majukumu waliyopewa kisheria ni kuwa na mkutano rasmi wa mara kwa mara na wadau wao wakiwemo wafanyabiashara wanaoingiza nchini bidhaa zinazosajiliwa na TBS.
The post Bidhaa za vyakula zisikidhi vigezo hazisajiliwi TBS first appeared on Millard Ayo.
Β