Na Farida Mangube, Morogoro Tanzania imetajwa kuwa na fursa kubwa ya kuongeza usalama wa chakula na kukuza uchumi kupitia sekta ya kilimo endapo wakulima watahamasika kulima kilimo cha kisasa kinachojali mazingira kwa kutumia teknolojia mahiri zinazowezesha uzalishaji mkubwa kwenye eneo dogo katika kipindi ambacho mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuathiri sekta ya kilimo nchini.Kauli hiyo imetolewa na wataalam pamoja na wadau mbalimbali wa kilimo, mazingira, uchumi, mifugo na mipango ya maendeleo waliokutana mjini Morogoro kwa lengo la kujadili kupitia mradi wa uchumi wa kijani jumuishi (Inclusive green economy – IGE) unaotekelezwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ufadhi wa shirika la misadaMradi huu umejikita kutoa uelewa kwa wakuu wa idara ambao wanatunga na kusimamia sera ambao wanapatiwa mafunzo ya namna gani wanatumia sera zilizopo kueleta maendeleo bila ya kuharibu mazingiraMkuu wa Idara ya Kilimo, Uchumi na Biashara wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Innocensia John, amesema njia sahihi ya kuendeleza kilimo cha kisasa kinachojali mazingira ni kuwahamasisha wakulima kupanda mazao yanayohimili ya ukame kama mikunde, mtama na mihogo pamoja na kutumia teknolojia za kuongeza tija.“Endapo wakulima wataendelea kupanda mazao ya asili yenye uwezo wa kustahimili ukame, watakuwa na uhakika wa chakula na pia watazalisha mazao mengi katika eneo dogo. Hii ndiyo njia sahihi ya kujenga ustahimilivu kwenye kilimo,” alisema Dkt. Innocensia.Aidha asemema mabadiliko ya tabianchi yameongeza hitaji la kubadili mfumo wa uzalishaji ili kulinda mazingira na kuzuia upotevu mkubwa wa mazao ambao kwa sasa unaathiri uwezo wa nchi kuzalisha vya kutosha.Kwa upande wake, Dkt. Aloyce Hepelwa Msimamizi wa Mradi wa IGE kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema mradi huo unalenga kuziwezesha jamii kutumia rasilimali kwa tija bila kuathiri mazingira, ikiwa ni sehemu ya kuunganisha kilimo cha kisasa na ujenzi wa uchumi wa kijani.“Mradi wa IGE umejikita katika kuwezesha jamii kupitia watunga sera kutumia rasilimali kwa tija bila kuathiri mazingira. Tunatarajia kuona ongezeko la uzalishaji, uhifadhi wa mazingira na matumizi endelevu ya ardhi ifikapo mwisho wa mradi,” alisema Dkt. Hepelwa.Mradi huo utakamilika mwaka 2027 una nafasi ya kuchochea mageuzi ya kilimo nchini kwa kuongeza maarifa, kubadili mtazamo wa vijana kuhusu kilimo cha kisasa na kuimarisha maamuzi ya sera kwa ushahidi wa kitaalamu.Bw. Vedastus Sitta ni mwakirishi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango, amesema kuwa kilimo mahiri ni sehemu muhimu ndani ya mpango mpana wa mageuzi ya kilimo unaobebwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na mpango wake wa miaka 25 utakaonza 2026 hadi 2051.“Kilimo mahiri ni eneo dogo lakini muhimu katika mageuzi ya kilimo ambayo dira imeyabainisha. Bila kilimo cha kisasa kinachozingatia utunzaji wa mazingira, hatutaweza kuongeza uzalishaji, kuwaingiza vijana wengi kwenye kilimo au kupanua mauzo yetu nje ya nchi,” alisema Sitta.Amesema hatua zinazochukuliwa na taasisi kama UDSM kupitia mradi wa IGE zinaonesha kuwa utekelezaji wa dira umeanza kabla ya muda, jambo linalotoa matumaini ya kujenga taifa lenye uchumi shindanishi, jumuishi na linalotumia ardhi kwa tija.“Nawapongeza wadau wote kwa kuanza utekelezaji kabla ya muda rasmi. Tunaomba vijana kujitokeza kwenye kilimo cha kisasa kinachotumia eneo dogo kuzalisha zaidi ili taifa lipate chakula cha kutosha na kuongeza pato la kigeni,” aliongeza. Read More
Na: OWM – KAM,Dar es Salaam Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo ameitaka Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuhakikisha programu za kutoa elimu kwa Wajasiriamali wanaofanya biashara ndogo ndogo zinakuwa endelevu ili kuwajengea uelewa wa vihatarishi vilivyopo katika shughuli wanazozifanya. Mhe. Read More
*Awekea mkazo upatikanaji wa ajira, huduma za kijamii na nishati nafuu *Apongeza PURA na TPDC kwa jitihada wanazofanya katika utafiti na uendelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia *Asisitiza mazingira rafiki ya uwekezaji Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba amefanya ziara katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Read More
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amekutana na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kuwapongeza kwa jitihada wanazoendelea kufanya katika utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za mafuta na gesi asilia nchini.Mkutano huo umefanyika tarehe 8 Desemba, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa TPDC jijini Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kujadili mikakati ya TPDC. Pamoja na mambo mengine Mhe.Salome ameelekeza Menejimenti ya TPDC kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi asilia majumbani na ujenzo wa vituo vya gesi asilia kwenye vyombo vya moto (CNG) ili Watanzania waendelee kunufaika zaidi na rasilimali hiyo muhimu.Aidha, amesisitiza kuwa miradi ya utafiti na uendelezaji wa gesi asilia, ikiwemo mradi wa LNG kuanza kushika kasi baada ya majadiliano kukamilika ili kuongeza tija katika uwekezaji na kuhakikisha nchi inanufaika kikamilifu na rasilimali zake.Katika hatua nyingine, Mhe.Naibu Waziri ameipongeza TANOIL ambayo ni kampuni tanzu ya TPDC kwa kuendelea kuwekeza kwenye biashara ya mafuta huku ikiwakilisha Kampuni ya kizawa lakini pia kuendelea kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta ya kutosha muda wote. Read More
Na Mwandishi wetuTimu ya Dar City kwa upande wa wanaume na Fox Divas kwa upande wa wanawake zimetwaa ubingwa wa mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu Tanzania (betPawa NBL 2025) yaliyomalizika Jumamosi kwenye uwanja wa Chinangali, mkoani Dodoma.Dar City ilitwaa kombe hilo baada ya kuichakaza Kisasa Heroes kwa pointi 80-51 wakati Fox Divas iliisambaratisha timu ya Vijana Queens kwa pointi 65-57.Hii ni mara ya pili mfululizo kwa timu za Dar City na Fox Divas kutwaa Ubingwa wa ligi ya betPawa NBL. Kwa mujibu wa rekodi za mashindano hayo, Dar City na Fox Divas kila mmoja zimejizolea zawadi nono kupitia mpango wa Locker Room Bonus (LRB) ya betPawa ambapo kila timu imejishindia Sh20.1 milioni kwa kushinda mechi zote za mashindano hayo.Timu zilizofuatia kulipwa fedha nyingi kupitia LRB ni Dodoma Spurs na JKT kwa upande wa wanaume ambapo kila moja ilishinda Sh15.6 milioni huku timu za Kisasa Heroes na Vijana Queens zilishinda kiasi cha Sh13.4 milioni kila moja.Timu za wanawake za JKT Stars na DB Lioness kila moja ilipata Sh11.2 milioni..Fedha hizo zililipwa moja kwa moja kwa Wachezaji na makocha kupitia simu zao za mikononi. Lengo ni kuwanufaisha na kutambua bidii zao kwa kushinda mechi.Mbali ya kuzoa fedha nyingi katika LRB, Dar City na Fox Divas walizawadiwa pia Sh 2.5 millioni kila moja kutoka betPawa kwa kuwa washindi wa jumla.Washindi wa pili wa mashindano hayo walizawadiwa Sh1.5 millioni na timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu, zilizawadiwa Sh500,000.Timu ya Bright Queens ya Dodoma ilishinda zawadi ya timu yenye nidhamu kwa upande wa wanawake wakati kwa wanaume timu ya Manyara ilishinda zawadi hiyo.Katika zawadi za mchezaji mmoja mmoja, Evelyne Nakilingi wa Fox Divas alishinda tuzo ya mchezaji bora na kuzawadiwa Sh500, 000 ambapo kwa wavulana zawadi hiyo ilikwenda kwa Romis Bujeje wa Kisasa Heroes.Pia Ekone Brenda wa Fox Divas alishinda zawadi ya mfungaji bora huku zawadi ya beki bora ilikwenda kwa Taudensia Katumbi wa DB Lioness na zawadi ya mchezaji bora chipukizi (best rookie) ilichukuliwa na Pendo Laizer wa Orkeeswa. Zawadi ya kocha bora kwa timu za wanawake ilikwenda kwa Bariki Kilimba wa Fox Divas. Kwa upande wa wanaume, zawadi ya mfungaji bora ilibebwa na Cheikh Dialo wa Dar City ambapo zawadi ya beki Bora ilichukuliwa na Mathew Mmasi huku tuzo ya mchezaji chipukizi ilikwenda kwa Feisar Mlanzi wa timu ya Pamoja na kocha bora ni Mohamed Mbwana wa timu ya Dar City. Washindi wa tuzo zote kwa wanawake na wanaume walizawadiwa kila mmoja sh300,000.Mbali na zawadi hizo, wachezaji na makocha mbalimbali walikuwa wanazawadiwa fedha kupitia Locker Room Bonus (LRB) Sh140,000 kila mmoja kutoka chapa ya betPawa ambayo ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo.Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo, Waziri wa Madini Anthony Mavunde alipongeza washindi na timu zote zilizoshiriki katika mashindano hayo yaliyokuwa na hamasa kubwa.“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nawapongeza wadhamini wakuu betPawa ambapo kwa kupitia mpango wa Locker Room Bonus (LRB) umeyafanya mashindano haya kuwa na ushindani mkubwa,” alisema Mavunde.Vilevile aliishukuru Azam TV kwa kuhakikisha Watanzania wote nchini wana kufuatilia mashindano hayo kwa ubora wa kimataifa. Kwa upande wake, Mratibu wa Masoko wa chapa ya betPawa wa Afrika Mashariki Nassoro Mungaya naye alimpongeza Waziri Mavunde na serikali kwa ujumla kwa kuchangia maendeleo ya michezo nchini na kuwavutia wadhamini kama kampuni yao.Mungaya alisema kuwa betPawa imeendelea kuwa mshirika wa karibu wa mpira wa kikapu nchini, na msimu huu wamewekeza Sh317 milioni kwa ajili ya ligi ya NBL.“Kipengele kikubwa kinachotambulisha udhamini wetu ni Locker Room Bonus (LRB) – mfumo wa kipekee barani Afrika unaowalipa wachezaji Sh140,000 papo hapo baada ya kila ushindi.Tumeona kwa macho yetu namna LRB ilivyobadilisha ari ya wachezaji, kuongeza ushindani, na kuleta hamasa toka hatua za makundi hadi playoffs. Tunajivunia kuona uwekezaji huu umetoa matunda kwa timu bora kwani mchezo umeimarika, na wachezaji wamethaminiwa, kwa kupata LRB, ” alisema Mungaya.Alisema kuwa chapa yao pia imechangia Sh13 milioni kwa ajili ya zawadi za washindi na tuzo mbalimbali. “Unaweza kuona jinsi gani chapa ya betPawa ilivyo uthaminisha mpira wa kikapu. Uwekezaji wetu si kwenye ligi tu, pia ni uwekezaji kwa vijana, vipaji na mustakabali wa michezo nchini,” alisema.Alisema kuwa Tanzania ina historia kubwa ya vipaji katika mpira wa kikapu na betPawa imejipanga kuendelea kuwa sehemu ya safari ya kukuza mchezo huu kwa muda mrefu kwa kuleta ubunifu, motisha, na kwa kuzingatia ustawi wa mchezaji.Waziri wa Madini Anthony Mavunde(wanne kutoka kushoto waliosimama) na mratibu wa Masoko wa betPawa wa Afrika Mashiriki, Nassoro Mungaya (wa pili kushoto) wakimkabidhi kombe la ubingwa wa klabu bingwa ya Tanzania “betPawa NBL” nahodha wa timu ya Dar City Amini Mkosa (wa tano kushoto) mara baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Kisasa Heroes uliofanyika kwenye uwanja wa Chinangali, Dodoma. Mratibu wa Masoko wa Afrika Mashiriki wa chapa ya betPawa, Nassoro Mungaya (kushoto) wakimkabidhi kombe la ubingwa wa klabu bingwa ya Tanzania “betPawa NBL” nahodha wa timu ya Fox Divas mara baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Vijana Queens uliofanyika kwenye uwanja wa Chinangali, Dodoma. Waziri wa Madini Anthony Mavunde akihutubia mara baada ya fainali ya mashindano ya klabu bingwa ya Tanzania “betPawa NBL” yaliofanyika kwenye uwanja wa Chinangali, Dodoma. Wachezaji wa timu ya Fox Divas wakipozi mara baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa la mashindano ya betPawa NBL yaliyomalizika mkoani Dodoma.Wachezaji wakichuana katika mechi ya fainali ya mashindano ya betPawa NBL kati ya Fox Divas na Vijana Queens Wachezaji wakichuana katika mechi ya fainali ya mashindano ya betPawa NBL kati ya Dar City na Kisasa Heroes Read More
NA Sophia Kingimali. WAHITIMU 121 wa Chuo cha Ufundi Stadi, Furahika(VETA) wametakiwa kuzingatia maadili wanapokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo ili kupata fursa ya kupata ajira. Pia,wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanapeleka watoto wao kwenye chuo hicho ili waweze kupata mafunzo ya ufundi stadi ili waweze kujiajili na kuounguza wimbi la vijana waliopo mtaani Read More
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.patrobas Katambi akizungumza kwenye mahafari ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mwanza Wahitimu wakiwa katika eneo la sherehe za mahafali. Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Mwanza Profesa Edda Lwoga akizungumza kwenye mahafali ya 60 ya chuo hicho yanayofanyika kwa mara ya18 Read More
NA MWANDISHI WETUWAHITIMU 121 wa Chuo cha Ufundi Stadi, Furahika wametakiwa kuzingatia maadili wanapokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo ili kupata fursa ya kupata ajira Mwenyekiti wa Bodi chuo hicho, Suddy Kassim Suddy ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tabata, ametoa wito huo kwa wahitimu hao wakati wa mahafali Chuo hicho Kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam."Maisha ni yetu mchakato ili ufanikiwe kunahitahi subira, uvumilivu na kuzingatia maadili ya kazi na kutojiingiza katika kwa vitu visivyo na maadili.Amesema kuwa maadili katika kazi ndio msingi wa kupata fursa ya kupata ajira yenye staha. "Msiende na mambo mawili mawili yatakayoharibu mwenendo wenu wa maisha, pia mnatakiwa kuangalia kwamba mmetoka katika familia gani, mkienda kufanya tofauti mtawaumiza wazazi wenu kwani wanamatarajio makubwa kwenu baada ya kuhitimu masomo, wakiamini mnakwenda kuwa msaada kwao," amesema.Ameongeza kuwa mwajiri hawezi kumuajiri mtu mwenye tabia za uzinzi, wizi na nyinginezo zisizo na maadili mema.Kuhusu mahitaji ya chuo, hicho ikiwemo upungufu wa vifaa vya kufundishia, ikiwemo kompyuta, cherehani ameahidi kulifanyia kazi kwa kuzungumza na wadau ili kuondoa changamoto hiyo.Naye Mkuu wa Chuo, hicho Aliko Mongele, amesema kuhitimu kwa wahitimu hao katika fani za hotel, Umeme, Bandari, air ticket, ICT, udereva na nyinginezo inatoa fursa ya kusajili wapya kwa muhula mpya utakaonza Januari.-Ameongeza kuwa kwa muhula mpya wa Januari wataanzisha kozi mpya ya ufundi bomba na kutoa wito kwa wazazi kuwapeleka vijana wao kuweza kusoma kozi hiyo na nyinginezo ili kuachana na umasikini.Pia muhimu wa kozi ya sekretal, Laura Matechi amesema anashukuru kufanikisha ndoto yake na sasa anaamini anakwenda kuitumia ili kufanya vema katika maisha yake na kuondokana na utegemezi.Pia muhitimu, Moses Victor, ametoa wito kwa vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto kadhaa wajitokeze kwenye Chuo hicho ili wapate elimu bure bila malipo ingawa wanacholipi na ada ya mtihani 50,000 na fomu pekee.Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Ufundi, Stadi Furahika na Diwani wa Tabata Suddy Kassim Suddy akizungumza katika mahafali ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi, Stadi Furahika David Msuya akizungumza mikakati ya Chuo katika mahafali ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo cha Furahika Aliko.Mmongele akizungumza mipango mikakati ya Chuo katika.kutanua fani zenye fursa ya ajira katika Mahafali ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam. Read More
Toyota Land Cruiser 300 (LC300) imekuwa gumzo barani Afrika tangu kuingia sokoni, ikiwa imebeba jina kubwa la uimara na uwezo uliotokana na historia ya zaidi ya miaka 70. Ndani ya familia hii, kuna matoleo matatu makuu ambayo watumiaji wengi husikia lakini hawajazoea kuyatofautisha kwa undani: GX-R, GR-S na ZX. Kila moja limebuniwa kwa malengo tofauti—kutoka
The post Usiyoyajua Kuhusu Toyota Land Cruiser Gx-R, Gr-S Na Zx (Lc300 Series) appeared first on Global Publishers. Read More