Fundi anayejenga mradi wa maji wa Kilindi-Barabara kata ya Matiri Halmashauri ya Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma Stanley Mlelwa wa pili kushoto akimuonyesha Mwenyekiti wa kijiji cha Barabara Ebhati Kapinga wa pili kulia,maji ya bomba yatakayosambazwa kwa Wakazi wa kijiji na Kilindi wapatao zaidi ya 3,800 ambao tangu Uhuru hawajawahi kupata maji ya bomba,kulia Afisa Uhusiano wa Ruwasa Mkoa wa Ruvuma Geddy Ndimbo(Picha na Muhidin Amri). Fundi anayejenga mradi wa maji wa Kilindi-Barabara kata ya Matiri Halmashauri ya Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma Stanley Mlelwa wa pili kushoto,na Afisa Uhusiano wa Ruwasa Mkoa wa Ruvuma Geddy Ndimbo kulia,wakimsikiliza Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Barabara kata ya Matiri Halmashauri ya Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma Ebhati Kapinga wa pili kulia,baada ya Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(Ruwasa) kuanza kutekeleza mradi wa maji ya bomba utakaonufaisha Wakazi wa kijiji hicho na Kilindi. Baadhi ya mabomba yatakayotumika kusambaza maji safi na salama kwa Wakazi wa kijiji cha Barabara kama yanavyoonekana. ………. Na Muhidin Amri, Mbinga WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA)Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma,upo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Kilindi-Barabara unaotarajiwa kumaliza kabisa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama. Wanufaika wa mradi huo ni Wananchi zaidi ya 3,800 wa Kijiji cha Kilindi na Barabara,ambao kwa muda mrefu hawana huduma ya maji ya uhakika, badala yake wanatumia maji kutoka kwenye visima vya asili,mito na mabonde. Meneja wa RUWASA Wilayani Mbinga Mashaka Sinkala alisema,mradi huo unatekelezwa kwa kutumia mafundi wa ndani na utakamilika mwishoni mwa mwezi huu na gharama za ujenzi wake ni Sh.milioni 68. Akizungumzia kuhusu miradi... Read More







