Mkurugenzi Mtendaji kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba Mosi, 2024 wakati wa kutangaza kongamano la Tanzania Japan katika Miundombinu. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Japan, Baraka Luvanda.
Balozi wa Tanzania Nchini Japan, Baraka Luvanda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba Mosi, 2024 wakati wa kutangaza kongamano la Tanzania Japan katika Miundombinu. na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri
KONGAMANO la Tanzania Japan kufanyika Oktoba 3,2024 jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba Mosi, 2024 Balozi wa Tanzania Nchini Japan, Baraka Luvanda amesema amekuja na washiriki wa Makampuni 60 kutoka taasisi ya Japan Africa Infrastructure Association (JAIDA)ambao wamekuja kwaajili ya kuangalia fursa za Uwekezaji zilizopo hapa nchini lakini pia fursa za kushirikiana na Watanzania katika utekelezaji wa Uwekezaji wa namna mbalimbali kwenye miundombinu n sekta zinazozunguka miundombinu.
Amesema Wanachama hao wa JAIDA watakutana na wadau mbalimbali wa Ujenzi wa Miundombinu hapa nchini ili kubadilishana uzoefu ili kuweza kutekeleza miradi ambayo itakuwa inapatikana nchini.
Amesema Ujio wa wanachama wa JAIDA ni juhuzi za kampeni iliyofanyika Mei na June 2024 nchini Japan na matokeo ya kampeni hiyo yameanza kuonekana tangu Julai kwa kupata mrejesho kutoka kwa wawekezaji wenyewe.
Amesema kupitia kampeni hiyo Japan kwa kupitia wenye mitaji binafsi pamoja na Serikali kuchangia katika mitaji hiyo wao ndio wawe vinara wa kutengeneza Miundombinu ambayo ni ya muda mrefu ambayo itaakisi aina ya miundombinu ambayo Japan wameweza kuijengakutokana na majanga kama tetemeko la Ardhi kwa kujenga miundombinu ambayo ni bora.
“Tunaamini baada ya hapo lile kufikia Januari Wawekezaji wanaweza kuongezeka.”
Kwahiyo Kampuni hizo zinazoshughulikia m Miundombinu ya Barabara, Viwanja vya ndege na Bandari.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji kituo cha uwekezaji Tanzania -TIC, Gilead Teri amewahimiza wakulima Nchini Tanzania kujikita katika zao la kahawa kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa katika Taifa la Japan.