Na WAF -DODOMA
Kamati ya Kudumu ya Bunge na Masuala ya Ukimwi chini ya Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Bernadetha Mshashu imeyataka Mabaraza ya maabara na famasi kuzingatia ubora wa huduma na mafunzo yatolewayo kwa wataalamu wa kada hizo.
Mhe. Bernadetha ameyasema hayo leo octoba 17, 2024 wa uwasilishwaji wa taarifa ya mabaraza ya maabara na ukunga kilichofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma
“Vipimo vya maabara ni muhimu lakini pia watoa dawa au wafamasia wanaotoa dawa bila karatasi ya daktari si sawa mnapaswa kuliangalia hilo kwani huweza kusababishia mgonjwa usugu wa dawa mwilini na kuleta athari,” mesema Mhe. Bernadetha
Mhe. Bernadetha ametoa pongezi kwa mabaraza ya maabara na famasia kwa kuwa na mafunzo endelevu kwa wataalam, ambapo mafunzo hayo yanawawezesha wataalam kuzingatia kanuni, sheria na miiko ya taaluma zao.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeamua kuweka mifumo ambayo itaweza kusimamia na kufanya uchunguzi kwenye maabara juu ya vipimo vinavyofanyika maabara moja na maabara nyingine na kuhakikisha matokeo ambayo mgonjwa ataambiwa maabara moja ni hayo hayo ambayo atakutana nayo katika maabara nyingine kwani mnyororo wa tiba ni uchunguzi na unaanzia maabara.
“Kwenye mnyororo wa tiba maabara na famasi ni sehemu muhimu sana kwani inaanza na maabara inafatiwa na tiba ambapo ni lazima upitie famasi ili uweze kupewa dawa tiba ivyo kuangalia msingi wa maabara na kuzidi kuboresha huduma za maabara ni kitu cha muhimu sana,” amesema Waziri Mhagama
Aidha, Waziri Mhagama ameongeza kuwa maabara ya Taifa imepewa hadhi ya kuwa kituo muhimu cha kutoa mafunzo ya ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi ili kuongeza usalama kwa afya za wananchi.