NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Takwimu zinaonyesha kuwa ajali nyingi za barabarani nchini zinatokana na kutofuatwa kwa sheria za barabarani, madereva wasio na weledi na kitendo cha kutozingatiwa maswala ya kiusalama kwa vyombo vya usafirishaji ndio vyanzo vikuu vya ajali hizo.
Kwa mjibu wa ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu( NBS) na jeshi la Polisi, Katika kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2023 jumla ya matukio 3,171,806 ya Usalama Barabarani yaliripotiwa katika vituo mbalimbali vya Polisi huku watu Watu 1,645 wakiripotiwa kupoteza maisha na wengine 2,686 walijeruhiwa ndani ya kipindi hicho.
Matukio hayo yameifanya kampuni ya Abood ( Abood Grop Company) kuwalejesha darasani madereva wake wanaofanya safari za kila siku kusafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine nchini, lengo likiwa ni kupunguza ajali zinazoepukika hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Moles masala ni msimamizi wa Mabasi kampuni ya Abood kizungumza na Waandishi wa Habari amesema lengo la kapuni hiyo ni kuwatoa madereva wake kuendesha magari kwa mazoea badala yake itakuwa inawajengea uwezo ili kuwawezesha madereva hao kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sharia za usalama barabarani.
“Kampuni ya Abood haitomvulia dereva yeyote atakaye kiuka kanuni na sharia za usalama barabarani.” Amesema Moles
Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhiti na Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Morogoro Bw.Andrew Mlacha amezitaka kapauni nyingine za mabasi kuiga mfano wa Abood kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa madereva wao ili kuwakumbusha mambo mbalimbali yanaweza kusababisha ajali.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Afya duniani (WHO) inabainisha kwamba nchi nyingi ikiwemo Tanzania zimeboresha sheria kama vile kuzuia mwendo kasi, ulevi na matumizi ya vifaa vya usalama kama matumizi ya mikanda, kofia za bodaboda yaani Helmet na hata viti maalumu kwa watoto.