Timu
ya mpira wa kikapu ya Dar City inaweza kutwaa ubingwa wa betPawa NBL
endapo itaibuka na ushindi katika mchezo wa pili uliopangwa kufanyika
usiku wa kesho, Novemba 19, 2024 kwenye Uwanja wa Chinangali Park,
Dodoma.
Dar City wana nafasi kubwa ya ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo wa pointi 97-48 kwenye mechi ya kwanza.
Katika
mchezo huo, Dar City ilitawala kila robo ya mchezo, wakiongoza 29-16
kwenye robo ya kwanza, 15-13 kwenye ya pili, na 31-7 kwenye ya tatu,
hali iliyowaacha ABC bila nafasi ya kurejea mchezoni.
Timu hiyo ilihitimisha ushindi wao kwa 23-12 kwenye robo ya mwisho.
Dar
City iliongozwa na wachezaji wake Shin Brownlee, Hasheem Thabeet Manka,
Amin Mkosa, Gilbert Nijimbere, na Alinani Andrew ambao walionyesha
uwezo wa hali ya juu na kuiwezesha timu hiyo kukaribia kutwaa taji la
betPawa NBL na kufuzu kushiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL)
mwakani.
ABC, ambao wamefika fainali za NBL kwa misimu minne
mfululizo, wanahitaji ushindi usiku wa leo ili kurejesha matumaini yao
ya kutwaa taji.
Historia yao ina mafanikio makubwa, ikiwemo
ubingwa wa mwaka 2021 huko Arusha na nafasi ya pili ambapo, mwaka jana,
walishindwa kutwaa taji hilo baada dhidi JKT Stars huko Dodoma.
Kwa upande wa wanawake, BD Lioness na Fox Divas wamefuzu fainali baada ya ushindi wa kuvutia katika mechi za nusu fainali.
BD
Lioness waliwashinda mabingwa watetezi Vijana Queens kwa alama 59-40,
huku Fox Divas wakiibuka na ushindi wa 83-52 dhidi ya JKT Stars.
Timu hizo zote mbili zinatazamia kutwaa taji kwenye fainali zijazo.
Akugumzia
maendeleo ya michuano hiyo, Meneja wa Masoko wa Kanda ya Afrika
Mashariki wa betPawa, Borah Ndanyungu alisema kuwa hamasa imekuwa kubwa
hasa baada ya kuanzisha utaratibu wa kuwalipa wachezaji 12 na viongozi
wanne kila mmoja sh140,000 endapo timu itashinda mechi.
“Bonus
hii imeongeza msisimko kwenye mashindano. Tunatarajia mchezo wa
ushindani mkubwa usiku wa leo wakati wachezaji wa ABC wakijaribu kurejea
na kudai zawadi hiyo,” alisema.
betPawa imetenga Sh milioni 130
kwa ajili ya zawadi, ikiwemo Sh milioni 14 za pesa taslimu za ushindi,
huku kiasi kingine kikisaidia shughuli za utawala wa Shirikisho la Mpira
wa Kikapu Tanzania (TBF).
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TBF,
Mwenze Kabinda, alisifu maandalizi mazuri ya mashindano hayo,
akiwashukuru betPawa na wadhamini wengine kwa mchango wao.
Mechi
ya usiku wa leo inatarajiwa kuwa na nishati ya hali ya juu na msisimko
mkubwa wakati timu zote zinapopambana kutafuta ushindi kwenye fainali za
NBL.
wa mpira wa kikapu katika mechi tofauti za kuwania klabu bingwa ya
Tanzania (betPawa NBL 2024) yanayo endelea kwenye uwanja wa Chinangali
mkoani Dodoma.
wakifuatilia mashindano ya kuwania klabu bingwa ya Tanzania (betPawa
NBL 2024) ambayo yanaendelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.
wa Mvumi Rippers ya Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja. Timu hiyo
ilishiriki mashindano ya kuwania klabu bingwa ya Tanzania (betPawa NBL
2024) ambbayo yanaendelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.
wa timu ya mpira wa kikapu ya wanawake ya Fox Divas wakifuatilia mechi
ya kuwania klabu bingwa ya Tanzania (betPawa NBL 2024) yanayo endelea
kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.
Wachezaji
wa timu ya Vijana Queens ambao wanashiriki mashindano ya klabu bingwa
ya mpira wa kikapu Tanzania (betPawa NBL 2024) yanayoendelea kwenye
uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.