Sekta ya michezo ya kubahatisha
nchini Tanzania imepiga hatua kubwa baada ya uzinduzi rasmi wa Bahati
Nasibu ya Taifa Tanzania iliyopata baraka kutoka zote kutoka kwa Mhe.
Hamad Chande, Naibu Waziri wa Fedha. Mpango huu, unaosimamiwa na ITHUBA,
Kampuni inayoongoza barani Afrika katika kuendesha michezo ya Bahati
Nasibu, unalenga kuleta mapinduzi katika sekta hiyo, kuchochea maendeleo
ya kitaifa, na kutoa fursa kwa kila Mtanzania kushiriki.
“Leo
ni siku ya kihistoria kwa Tanzania,” alisema Mhe. Chande wakati wa
hotuba yake. “Kwa kumkaribisha ITHUBA kama mwendeshaji rasmi wa Bahati
Nasibu ya Taifa, tunatoa kipaumbele katika suala zima la uvumbuzi,
uaminifu, na uwazi huku tukileta jukwaa litakalochochea ukuaji wa
uchumi, ajira mpya, na miradi ya maendeleo ya kitaifa kwa ajili ya
kuinua maisha ya wananchi.”
Fursa za Kusisimua za Michezo kwa
Wote; Bahati Nasibu ya Kitaifa itakuwa na mkusanyiko wa michezo
mbalimbali ya kuvutia iliyoundwa mahsusi kwa ajili ya kuwashirikisha na
kuwaburudisha Watanzania, ikiwa ni pamoja na LOTTO, TAMBA NA NAMBA,
SPIN4CASH, na TOBOA CHAP CHAP. Tiketi zinaanzia bei ya Shilingi 100 tu
za Kitanzania, kuhakikisha kila mtu anaweza kushiriki.
“Kila
tiketi itakayouzwa itachangia kuboresha michezo, elimu, na miradi ya
kijamii,” aliongeza Mheshimiwa Chande. “Bahati Nasibu ya Taifa hii ni
mfano wa jinsi michezo ya kubahatisha inavyoweza kutumika kama chombo
cha maendeleo endelevu huku ikiwaletea washiriki furaha.”
Ujumbe wa Afisa Mtendaji Mkuu wa ITHUBA Group, Bi. Charmaine Mabuza,
ulisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika maendeleo ya Tanzania.
“ITHUBA inajivunia kushirikiana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania (GBT) kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa. Dira yetu ni kutoa
uzoefu wa hali ya juu wa michezo ya Bahati Nasibu kwa uwazi,
kuburudisha, na kusaidia maendeleo endelevu. Bahati Nasibu hii si tu
kuhusu michezo bali pia ni sehemu ya kuinua jamii zetu na kuwekeza
katika mustakabali bora wa Tanzania.”
Kwa usimamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bahati Nasibu ya Taifa
itazingatia viwango vya juu vya uwazi na haki. Balozi Modest J. Mero,
Mwenyekiti wa GBT, alibainisha umuhimu wa uadilifu katika mpango huu.
“Sifa ya ITHUBA katika uwajibikaji wa kimaadili na uvumbuzi unaifanya
Kampuni hii kuwa mshirika bora. Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
itahakikisha Bahati Nasibu ya Taifa inafanya kazi kwa uwazi na uaminifu
kama jukwaa salama linalochangia malengo ya kiuchumi ya Tanzania,”
alisema Balozi Mero.
Bahati Nasibu ya Taifa inatarajiwa kuleta
mabadiliko makubwa katika sekta ya michezo ya kubahatisha nchini. Mapato
ya tiketi yatatumika kufadhili maendeleo ya michezo katika ngazi ya
msingi, uwezeshaji wa vijana, na miradi muhimu ya kijamii, kuimarisha
jukumu la Bahati Nasibu ya Taifa kama chombo cha maendeleo ya kijamii.
Baadhi
ya Michezo inayopatikana Kupitia Bahati Nasibu ya Taifa: LOTTO: Jakpoti
za kila siku zenye zawadi kubwa zinazobadilisha maisha.
TAMBA NA NAMBA: Mchezo wa haraka wa droo kila baada ya dakika 5.
SPIN4CASH: Michezo ya kushinda papo hapo na malipo ya haraka.
TOBOA CHAP CHAP: Michezo ya papo hapo yenye mada za kuvutia kama MFUGA KUKU na TUNDA KITMATI.
Fursa kwa Wadau Wote: Washiriki: Zawadi za zaidi ya dola milioni 60 zinatarajiwa kutolewa katika mwaka wa kwanza pekee.
Wauzaji na Washirika wa Biashara: Kamisheni za takriban dola milioni 6.6, pamoja na mafunzo na msaada wa kimasoko.
Vyombo vya Habari: Zaidi ya dola milioni 3.5 zimetengwa kwa masoko na matangazo, ikijumuisha fursa za kipekee za maudhui.
Bahati Nasibu ya Taifa itahakikisha ushirikishwaji wa kila mmoja wetu
kwa kutoa tiketi kupitia majukwaa ya kidigitali, huduma za simu, na
vituo vya rejareja kote nchini. Juhudi za kufikia maeneo ya vijijini pia
zimepangwa kuhakikisha kuwa hata jamii za pembezoni zinaweza kushiriki
na kufaidika.
“Bahati Nasibu ya Taifa ni alama ya mshikamano,
uwezeshaji, na maendeleo,” alisema Bi. Mabuza. “Kwa pamoja,
tunatengeneza urithi wa ustawi wa pamoja kwa vizazi vijavyo.”