
Na Khadija Kalili Michuzi TV
WAZIRIwa Viwanda Dkt Selemani Jafo ametoa agizo kwa Mamlaka ya Maji Vijijini Ruwasa kuchimba Kisima kirefu Kata ya Bwama iliyopo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
Mhe.Dkt.Jafo ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ametoa agizo hilo alipofika Bwama kwenye hafla ya kuzindua Zahanati ya Bwama ambayo imekamilika na ameizindua Januari 24 na tayari kw a kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Ujenzi wa Zahanati hiyo umegharimu kiasi cha Mil.77 ulianza mwaka 2010.
Agizo la Mh.Dkt. Jafo amelielekeza kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Beatrice Dominic.
“Natoa agizo waambie Ruwasa waje wachimbe kisima Bwama wahangaike wawezavyo kuchimba kisima kirefu kwani ninafahamu sasa hivi Kuna juhudi mbalimbali zinafanyika” amesema Dkt.Jafo.
Alizungumza kuhusu ujenzi wa Zahanati hiyo ujenzi wa huo umetokana na nguvu za wananchi mfuko wa jimbo pamoja na serikali kuu.
“Mfuko wa jimbo umejenga zahanati nyingi Ila hapa Bwana mmefanya vizuri Sana nawapa pongezi kwa kujenga Jengo zuri” Dkt.Jafo.