





Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Endulen, wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwa njia ya filamu kuhusu elimu ya fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Kijiji cha Endulen, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Ngorongoro, Arusha)
Na. Saidina Msangi, WF, Ngorongoro, Arusha.
Wizara ya Fedha inaendelea na Program ya kutoa elimu kwa Umma ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo Sekta ya Fedha 2020/21 – 2029/30 ambapo unalenga kufikia wananchi asimia 80 hadi kufikia mwaka 2025/26 pamoja na utekelezaji wa Programu ya Elimu ya Fedha kwa Umma ya mwaka 2020/21 – 2025/26.
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, imeifikia jamii ya Wamaasai katika Kijiji cha Nainokanoka na Endulen katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha na kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini.