Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Dimwa akifafanya jambo katika kikao kilichowakutanisha Viongozi wa Veta Kanda ya Mashariki na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo huko Migombani Wilaya ya Mjini.
………………
Zanzibar. 18.02.2025.
Naibu katibu Mkuu wa Chama Cha cha Mapinduzi Zanzibar Dkt. Muhammed Said Dimwa ameupongeza ujumbe wa Veta kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia Vijana wa Zanzibar.
Dkt. Dimwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa Veta Veta Kanda ya Mashariki na Viongozi wa Idara ya Maendeleo ya Vija na Zanzibar huko Migombani Wilaya ya Mjini.
Amesma Zanzibar inategemea sana Mafunzo ya amali katika kuwawezesha Vijana ikiwa ni kutekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi kinaridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar katika kuwawezesha Vijana na kuahidi kushirikiana nao kwa hali na mali.
“Tutaendelea kuwasimamia na kuwapa moyo ili wazidi kufanya kazi kwani kufanya vizuri kwa Wizara na sisi tunapata jichwa kutokana na kuwa Wanatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi” alibainisha Dkt. Dimwa.
Mbali na hayo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab kukaa pamoja na Uongozi huo wa Veta ili kuweza kuendesha program zitakazowasaidia Vijana wa Zanzibar na kuweza kujiajiri, kuajiriwa na kupatiwa vyeti.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab ameupingeza Uongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa kuwashika mkono jambo ambalo limewawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Aidha Katibu Fatma, ametumia muda huo kwa kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanaia Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kupeperusha Bendera ya Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu.
Ujumbe huo wa Veta kutoka Kanda ya Mashariki umeongozwa na Mkurugenzi wa Kanda hiyo Muhandisi John Mwanja ambapo ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupiga hatua kubwa ya Maendeleo.
Hata ivyo ameishauri Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwatumia vijana wazalendo katika miradi ili waweze kupata ajira sambamba na kuwepo Umeme wa uhakika ili kuondosha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Imetolewa na Kitengo Cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano,