Mratibu wa Urasimishaji Ardhi Manispaa ya Ubungo Majaliwa Jafari Mwamba wakati akizungumza kwenye zoezi la clinic ya ardhi inayoendelea kufanyika katika viwanja vya Kimara stop Over ambayo imeanza tar 10 feb mpaka tar 24 mwezi huu.
Maafisa kutoka Manispaa ya Ubungo wakiwahudumia wananchi ambao wamejitokeza kwenye zoezi la clinic ya ardhi linaloendelea kufanyika katika viwanja vya Kimara stop Over ambayo imeanza tar 10 feb mpaka tar 24 mwezi huu
Baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kwa wingi kwenye zoezi la clinic ya ardhi linaloendelea kufanyika katika viwanja vya Kimara stop Over ambayo imeanza tar 10 feb mpaka tar 24 mwezi huu.
………………………
NA MUSSA KHALID
Takriban wananchi 1074 kutoka Wilaya Ubungo Mkoani Dar es salaam wamehudhuria ArdhiClinic huku 771 wakifunguliwa majalada kwa ajili ya utoaji hati na 652 wamepata hatimikili ya ardhi.
Pia imeelezwa katika utatuzi wa migogoro ya ardhi zimepokewa changamoto mbalimbali za migogoro ya Ardhi 83 na 52 zimepatiwa majawabu.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Urasimishaji Ardhi Manispaa ya Ubungo Majaliwa Jafari Mwamba wakati akizungumza kwenye zoezi la clinic ya ardhi inayoendelea kufanyika katika viwanja vya Kimara stop Over ambayo imeanza tar 10 feb mpaka tar 24 mwezi huu.
Majliwa amesema kuwa katika zoezi hilo wanatoa elimu kwa jamii ikiwemo kutoa hati na hata utatuzi wa migogo na masuala mbalimbali ya ardhi
‘Vilevile tumetoa elimu mbalimbali kwa wananchi 1074 katika zoezi hili ambalo linaendelea na leo tupo katika siku ya kumi na zoezi letu linatarajiwa kumalizika tarehe 24/2/2025”amesema Majaliwa
Aidha amesema kuwa mpaka sasa malengo yao waliyojiwekea wameyatimiza kwa asilimia 80 na kwa siku zilizosalia watahakiksha wanakamiliza malengo yao zaidi.
‘Mategemeo ya Wilaya mpaka zoezi kukamilika ni kutoa haki hati 1500 na hivyo niwahamishe wananchi ambao badoi hawajajitokeza wafike wakiwa na namba zao za viwanja,wawe na fomu za kisheria wahakikishe wamepata fomu namba 19,wawe wamepata fomu za mipaka na kiapo na wawe na namba za nida’ameendelea kusisitiza Majaliwa.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao wameshiriki katikam zoezi hilo akiwemo Lupakis Jonas pamoja na Gerald Lyimo wameipongeza serikali kwa kuwapelekea maafisa katika clinic hiyo kwa itasaidia kuwarahisishia katika masuala mbalimbali.
Wameomba zoezi hilo kuwa ni endelevu katika wilaya hiyo kwani baadhi ya wananchi hawajazifuatilia hati hizo ili waweze kurasimisha ardhi zao.
Mratibu huyo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la ardhi clinic ili kuweza kupata huduma hiyo kwa haraka kutokana na shughuli zote kupatikana kwa wakati mmoja.